Wakili Sharon Korir mwathiriwa wa Fistula, anasema alipitia nyingi baada ya kugundua anaugua Fistula ukiwamo unyanyapaa kutoka kwa familia na jamaa zake. Anasema alianza kuugua baada ya kujifungua mwanawe wa pili. Baada ya kudhalilishwa na hata kutengwa na mumewe alipokuwa na Fistula, Wakili Korir hakukataa tamaa aliamua kumwelezea shemejiye kuhusu tatizo hilo kisha akapata matibabu. Amezungumza na Carren Papai kuhusu jinsi mambo yalivyoanza, akiwa hospitalini na kipindi cha kupona katika sehemu hii ya kwanza ya Kisa Changu Podcast